Tulieleza katika video zilizopita kwamba saratani huanza wakati kundi la seli mwilini linapoanza kukua na kugawanyika nje ya udhibiti. Pia tulieleza kuwa hii inaweza kutokea sehemu yoyote ya mwili na kusambaa sehemu nyingine pia pale inapokuwa saratani. Kwa hiyo, saratani hupewa jina la sehemu ya mwili ambapo ilianzia mara ya kwanza, hata inaposambaa sehemu nyingine baadaye.
Kwa hiyo, kama saratani inaanzia kwenye ovari, basi inaitwa saratani ya ovari, ambayo ni mada yetu kwa makala hii.
Saratani ya Ovari ni nini?
Ovari ni maeneo ya uzalishaji wa mayai kwa wanawake, pia ni chanzo kikuu cha homoni za estrogen na progesterone. Mayai yanayozalishwa na ovari husafiri kupitia mrija wa fallopian hadi kwenye mfuko wa uzazi ambapo hurutubishwa na kukaa kwenye mfuko wa uzazi na kutengeneza kijusi.